KUELEKEA mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga.....historia ya simba na yanga angalia hapa sylas tv
KUELEKEA mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga, kocha wa Simba Pierre Lechantre, amewataka wachezaji wake kuongeza umakini na kuhakikisha wanaitumia vizuri kila nafasi watakayoipata.
Simba na Yanga zimepiga kambi mkoani Morogoro kujiandaa na pambano hilo ambalo mshindi ndiyo anapewa nafasi kubwa kuwa bingwa wa msimu huu ambao unaelekea ukingoni.
Akizungumza gazeti hili, Lechantre alisema huo ni mchezo mgumu sana hivyo wanapaswa kuwa makini na kuitumia kila nafasi ambayo wataipata vinginevyo wanaweza kujuta kwenye majuto baada ya dakika 90.
“Mchezo mkubwa kama huo ni mara nyingi nafasi za mabao huwa chache hivyo naendelea kuzungumza na wachezaji wangu ili tuweze kuzitumia nafasi ambazo tutazipata ukizingatia ushindi ndiyo utatuhakikishia ubingwa wetu msimu huu,” alisema Lechantre.
Mfaransa huyo alisema kinachompa hofu kwenye mchezo huo ni kutokana na wapinzani wao kutotabirika kutokana na kikosi chao kubadilika mara kwa mara hivyo ni lazima waingie kwenye mchezo huo kwa tahadhari na kuwaheshimu.
Alisema anatambua kuwa ana kikosi bora ambacho kinaundwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa kuliko kile cha wapinzani wao, lakini hawapaswi kuwadharau kwa sababu kwenye soka chochote kinaweza kutokea kitu cha msingi kwao ni kucheza kwa makini na wachezaji wake kufuata kile atakacho waelekeza.
“Tumejipanga vizuri kiukweli wachezaji wangu wote wapo katika ari kubwa kuelekea kwenye mchezo huo naamini hawatoniangusha kwa sababu kitu cha msingi kwetu sote ni ubingwa na rekodi nzuri kwa kila mmoja wetu,” alisema.
Simba ndiyo wenyeji wa mchezo huo na wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa vinara kwa tofauti ya pointi 11 dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na pointi 48 huku wakiwa na michezo miwili nyuma.
historia ya simba na yanga
angalia hapa sylas tv
Post a Comment