Header Ads

Mkazi mmoja mkoani Kigoma aliyejulikana kwa jina la Ndimugwanko Mlovezi anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumpiga mkewe na kumuua.


Akizungumza na www.eatv.tv kuthibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Ottieno, amesema tukio hilo limetokea April 20 ambapo mwanaume huyo alimpiga mkewe Bi. Selina Simon hadi kumuua, akimtuhumu kwa nini anamzalia watoto wa kike pekee.
“Tukio limetokea tarehe 20 April saa moja na nusu jioni katika kijiji cha Itundiko, Kakonko, mama aniatwa Selina Simon mwenye miaka 35, aliuawa kwa kupigwa na mume wake Ndimugwanko Mlovezi mkazi wa kijiiji hicho hicho kwa kumpiga na fimbo maeneo mbali mbali ya mwili wake, chanzo kikubwa kilichopeleka kipigo hiko kulikuwa na ubishano mkubwa kati ya marehemu na mtuhumiwa, juu ya kumzalia watoto wa kike mfululizo bila kumzalia wa kiume,ndio chanzo cha kumpiga", amesema Kamanda Ottieno.
Kamanda Ottieno amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamni hapo kesho April 24 kujibu mashtaka yake yanayomkabili.
KILICHO JILI BUNGENI ANGALIA HAPA

No comments