Header Ads

Zuma,atangaza ndoa Bada Kigoli kumteka kimahaba






Taarifa hizo zimethibitishwa na mwenyewe mke mtarajiwa wa Zuma anayejulikana kwa jina la Nonkanyinso Conco, kupitia chombo cha habari cha Times live cha nchini Afrika Kusini.
“Ndio tunaoana, hayo ndiyo naweza kusema kwa sasa, nahitaji kutoa taarifa kabla sijafanya interview yoyote”, amesikika binti huyo akiuambia mtandao wa Times Live.
Habari zaidi zinasema kuwa binti huyo tayari ana mtoto mchanga aliyezaa na Jacob Zuma ambaye amezaliwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Jacob Zuma, April 12, na tayari mahali imeshatolewa.
Jacob Zuma ambaye ana miaka 76 mpaka sasa ameshaoa mara 6, na hii itakuwa ni mara ya 7 kufunga ndoa,
Tukio hilo limeonekana kuwakwaza wananchi wa Afrika Kusini na kutoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii, wakisema binti huyo ni mdogo sana kwa Zuma, kwani wana tofauti ya miaka 52.
Tazama baadhi ya maoni yao.

No comments