Papa Francis atoa wito wa amani kote duniani
Akianza na nchi anayopenda kutoa wito wa amani na inayokabiliwa na vita vya muda mrefu ya Syria," aliendelea katika eneo lote la mashariki ya kati, rasi ya Korea na sehemu za Afrika zilizoathirika na 'njaa, mizozo isiyokwisha na ugaidi."
Francis aliakisi mtazamo wake katika nguvu ya imani ya msingi ya Ukristo kwamba Yesu aliamka kutoka mautini baada ya kuteswa msalabani , katika ujumbe wake wa kila mwaka wa Pasaka unaojulikana kama "Urbi et Orbi" ama "kwa mji na dunia" unaotolewa katika kibaraza cha kanisa la Mtakatifu Petro Basilica katika uwanja wa kanisa hilo uliojaa watu pomoni.
"Unazaa matunda ya matumaini na utu ambako kuna udhalilishaji na kutengwa, njaa na ukosefu wa ajira; kule ambako kuna wahamiaji na wakimbizi, ambao kila mara wanakataliwa na utamaduni wa ubadhirifu katika siku hizi, na wahanga wa biashara ya madawa ya kulevywa , biashara ya kusafirisha watu kwa njia haramu na njia za utumwa wa kisasa, " Papa alisema.Kiongozi huyo wa kidini amesema ujumbe wa ufufuo unatoa matumaini katika dunia "inayokabiliwa na matukio mengi ya kutokuwa na sheria na matumizi ya nguvu."
Ametoa wito wa "kumalizwa kwa haraka " mauaji nchini Syria, akisisitiza kwamba misaada ipelekwe haraka kwa wanaoihitaji nchini humo na kutoa wito wa "hali inayokubalika ya kurejea na wale waliokimbia makaazi yao."
Papa pia amehimiza maridhiano nchini Israel na ana matumaini kwamba "kuheshimiana kutakuwapo badala ya utengano" nchini Yemen na katika eneo lote la Mashariki ya Kati.
Akigeukia barani Asia, Francis ana matumaini kwamba mazungumzo yanayoendelea yanaweza kuleta amani katika rasi ya Korea, na kuhimiza " wale ambao wanahusika moja kwa moja kuchagukua hatua za busara na utu kuhimiza kila jambo jema kwa watu wa Korea.
Kwa upande wa Ukraine, papa amehimiza hatua zaidi kuchukuliwa kuleta umoja katika taifa hilo lililogawika. Pia ametoa wito wa amani katika Sudan kusini na Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, akiitaka dunia kutowasahau wahanga wa mizozo hiyo, hususan watoto.
"Iwapo hakuna mshimano na wote wale waliolazimika kukimbia mataifa yao ya asili na ukosefu wa vitu muhimu vya kuwawezesha kuishi," Papa amesema mara kadhaa amekuwa msitari wa mbele katika utetezi wa wahamiaji na wakimbizi.
Mapema, mamia kwa maelfu ya waumini walipitia ukaguzi mkali wa usalama kuingia katika uwanja wa Mtakatifu Petro kuhudhuria sala ya Jumapili ya Pasaka iliyoongozwa na Papa, iliyofuatiwa na ujumbe wa "Urbi et OrbKiongozi wa kwanza wa kanisa hilo kutoka Amerika ya kusini amedokeza hususan matatizo nchini Venezuela, akieleza matumaini kwa nchi hiyo kwamba "itapata njia ya haki, amani na utu ili kuwa haraka juu ya mzozo wa kisiasa na kiutu ambao unaikumba nchi hiyo."
Post a Comment