Header Ads

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas leo anatarajiwa kuzuru kambi ya wakimbizi


Image result for jerumani Heiko Maas


Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas leo anatarajiwa kuzuru kambi ya wakimbizi pamoja na wanajeshi wa Ujerumani walioko Jordan katika siku ya pili ya ziara yake nchini humo. Kambi ya al-Azraq ni ya pili kwa ukubwa na inahifadhi wakimbizi 37,000.

 Kulingana na taarifa rasmi Jordan ina wakimbizi zaidi ya 600,000 kutoka Syria lakini kutokana na wengine kutoorodheshwa idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zadi hadi kufikia milioni 1.2. 

Maas pia anatarajia kutembelea kambi ya wanajeshi 300 wa Ujerumani walioko nchini Jordan na pia kuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Jordan Ayman Safadi na baadaye kukutana na mwana wa Mfalme Faisal bin Hussein ambapo watajili masuala kadhaa ukiwemo mgogoro wa Syria na Yemen.

siri ya uchawi angalia SYLAS TV


No comments