polisi nnchini kenya kuwa chapa wananchi
Kundi la wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa , limelaani
machafuko yaliyoambatana na msako wa polisi dhidi ya watu waliokuwa
wakiandamana kwa amani katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Wataalam hao
wameitaka mamlaka ya nchi hiyo kuchunguza madai ya matumizi ya nguvu
kupita kiasi na kukamatwa kiholela kwa waandamanaji na waandishi wa
habari na kutaka wote waliohusika kuwajibishwa.
Watu hao walikuwa wakiandamana kupinga madai ya ufisadi unaofanywa na
serikali wakati polisi walipotumia mabomu ya kutoa machozi na virungu
kuwatawanya ambapo watu kadhaa wameripotiwa kuumia au kuwekwa rumande
kufuatia tukio hilo la Novemba 3, mwaka huu.
Wataalamu hao wamesema kuingilia haki ya uhuru wa kuandamana kwa
amani ni suala lisilosameheka na hasa pale ambapo waandamanaji wanadai
uwajibikaji kutoka kwa serikali.
Post a Comment