Header Ads

Waumini wa dini ya kikristu wameaswa kusimama imara katika imani badala ya

Waumini wa dini ya kikristu wameaswa kusimama imara katika imani badala ya 

Image result for picha ya yesu









Waumini wa dini ya kikristu wameaswa kusimama imara katika imani badala ya kuyumba na kutetereka kutokana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.



Image result for picha ya yesu



Hayo yameelezwa Jana na Paroko wa Parokia ya ngokolo Padri Adolf Makandagu wakati akihubiri kwenye adhimisho la misa ya Jumapili kwenye kanisa kuu la Mama mwenye Huruma ngokolo mjini Shinyanga.

Amesema tabu,shida,matatizo na mahangaiko isiwe chanzo cha kutetereka kiimani, na badala yake wanapaswa kusali kwa kumtumainia mungu,ili waweze  kuyashinda majaribu na mitihani iliyopo mbele yao.

Padre Makandagu amesema wakristu wanapaswa   kuwa wavumilivu wenye kupenda kusoma biblia,kujifunza na kuyajua mafundiso ya mungu hali ambayo itawasaidia kusimama katika imani thabiti nakufata yote ambayo yesu aliwataka wafanye wanafunzi wake.

Amewakumbusha  waumini kuwa  wana wajibu wa  kuwarithisha watoto wao mila na desturi  zinazozingatia imani  na maadili ya kikristu,lakini pia umuhimu wa kusaidiana  na kuwaombea wengine wenye  mahangaiko badala ya kuwatenga na kuwabagua kutokana na madhaifu yao kwani watu wote nisawa 



                                                               








No comments