Header Ads

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kesho Jumamosi anatarajia kufunga Fainali za Michuano ya Vijana ya Mpira wa Kikapu

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kesho Jumamosi anatarajia kufunga Fainali za Michuano ya Vijana ya Mpira wa Kikapu ijulikanayo kama NBA Junior League katika Viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.


Image result for KIKWETE


Msimamizi wa Mpira wa Kikapu kwa Vijana Bahati Mgunda amesema, fainali hizo zitakazohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mchezo huo zitatanguliwa na Nusu Fainali.
Nusu Fainali itawakutanisha Tusiime dhidi ya DIS huku Lord Barden ikicheza dhidi ya shule ya Umoja wa Mataifa na mara baada ya hapo atatafutwa mshindi wa tatu huku ukichezwa mchezo wa All Stars ambao utawajumuisha wachezaji ambao wamechaguliwa katika mashindano hayo.
Mgunda amesema mara baada ya kukamilika kwa fainali hizo, katika mashindano hapo mwakani wanatarajia kuwa na timu za wanawake ambazo zitashiriki katika Ligi hiyo.


CHANZO EATV

No comments