Header Ads

YANGA KUSAJILI KOCHA MPYA

YANGA KUSAJILI KOCHA MPYA

Image result for PICHA YA YANGA


KOCHA mpya wa Yanga, Mzambia George Lwandamina anatarajiwa kutua nchini Jumatano baada ya kumalizana na klabu yake ya sasa, Zesco United ya kwao
Image result for PICHA YA YANGA


Justin Mumba na Katebe Chengo Mtendaji Mkuu wa ZESCO na Ofisa Habari wametoa taarifa ya kuachana na Lwandamina.

Lwandamina ambaye amekwishamalizana na uongozi wa Yanga jana aliiongoza Zesco United katika mechi ya Ligi Kuu ya Zambia dhidi ya Nkana FC na leo anatarajiwa kuwa na kikao na waajiri wake.

Uongozi wa Yanga unataka kumuondoa kocha Hans van der Pluijm na Wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo na kuwaleta Mzambia Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.

Hata hivyo, mpango huo unakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wadau wa timu hiyo na wapenzi wanaoamini Pluijm bao chaguo sahihi Jangwani.

Ikumbukwe wiki mbili zilizopita Pluijm alisusa kwa siku tatu kufanya kazi Yanga na kuwasilisha barua ya kujiuzulu baada ya kukerwa na taarifa za ujio wa Lwandamina.  

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba aliingilia kati suala hilo na kufanikiwa kumrejesha kazini Pluijm.

Waziri Mwigulu ambaye ni mpenzi na mwanachama wa Yanga, kwanza aliushauri uongozi kumrudisha Pluijm na baadaye akaenda kuzungumza na kocha huyo pia kumshauri akubali kurejea.
Baadaye akazikutanisha pande zote mbili, Pluijm na uongozi wa Yanga katika kikao ambacho inaelezwa makubaliano yalifikiwa kabla ya uongozi wa Yanga kumemuandikia barua Mholanzi huyo kumuomba radhi.


No comments